Rais Xi Jinping wa China asisitiza kushinda mapambano magumu dhidi ya ufisadi
2024-01-09 08:19:55| CRI

Katibu Mkuu wa Chama cha Kikomunisti cha China (CPC) na Rais wa China Bw. Xi Jinping ametoa wito wa kuendeleza mageuzi ya ndani ya Chama na kushinda mapambano dhidi ya ufisadi, magumu na yaliyodumu kwa muda mrefu.

Rais Xi, ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamisheni Kuu ya Jeshi, alitoa kauli hiyo wakati akihutubia kikao cha tatu cha Kamisheni Kuu ya 20 ya Ukaguzi wa Nidhamu ya CPC.

Baada ya jitihada za kupambana na ufisadi katika muongo uliopita wa zama mpya, ushindi mkubwa umepatikana kwenye vita dhidi ya ufisadi, na matokeo yake yamezidi kuimarika.

Hata hivyo Rais Xi pia ameainisha kuwa hali ya sasa bado ni mbaya na tete, na ametaka kufanywa juhudi zaidi ili kushinda vita hii ngumu na ya muda mrefu.