Jeshi la Israel laanza kipindi kipya kisicho na makali makubwa katika operesheni huko Gaza
2024-01-09 08:48:44| CRI

Msemaji wa Jeshi la Israel (IDF) Bw. Daniel Hagari amesema, jeshi hilo limeanza kipindi kipya kisicho na makali makubwa katika operesheni yake ya kijeshi dhidi ya kundi la Hamas huko Gaza.

Amesemaa IDF sasa inageukia “kufanya shambulizi la mara moja moja badala ya kudumisha mashambulizi makubwa”, huku akiongeza kuwa vita imebadilika.

Bw. Hagari amongeza kuwa Israel itatilia maanani mapigano dhidi ya kundi la Hamas katikati na kusini mwa Gaza, hasa karibu miji ya Khan Younis na Deir al-Balah, wakati likipunguza vikosi vyake huko Gaza.

Habari nyingine zinasema jeshi la Israel limetangaza kuwa limemuua ofisa wa kundi la Hamas aliyeongoza mashambulizi ya makombora dhidi ya Israel, Hassan Akasha, katika wilaya ya Beit Jann, kusini mwa Syria.