Msomi wa Zimbabwe: Nchi za Magharibi zina nia ya kusambaza habari zisizo za kweli za kuichafua China
2024-01-09 15:43:59| CRI

Hivi karibuni, Msomi wa Ulaya Bw. Jan Oberg alisema kuwa, bunge la Marekani lilipitisha muswada wa sheria wa kutenga dola za kimarekani bilioni 1.5 kwa miaka mitano mfululizo kwa ajili ya kuwafundisha waandishi wa habari wa nchi za Magharibi kuandika habari zisizo za kweli kuhusu China.

Mtaalamu wa uhusiano kati ya Zimbabwe na China Bw. Tichaona Zindoga amesema, nchi za Magharibi na vyombo vya habari vya nchi hizo zina nia ya kusambaza habari zisizo za kweli za kuichafua China, ikiwa ni pamoja na habari kuhusu Ukoloni Mamboleo wa China na mtego wa madeni wa China barani Afrika.

Kutokana na Pendekezo la Ukanda Mmoja na Njia Moja la China na Baraza la Ushirikiano kati ya China na Afrika (FOCAC), uhusiano wa kirafiki na ushirikiano kati ya China na Afrika umeimarishwa zaidi katika miaka ya hivi karibuni, lakini ushirikiano huo umekashifiwa na vyombo vya habari vya Magharibi kuwa ni “Ukoloni Mamboleo” barani Afrika, na mtego wa madeni kwa nchi za Afrika.

Bw. Zindoga akizungumzia suala hili, amesema anaamini kuwa Ukoloni Mamboleo wa China na mtego wa madeni barani Afrika ni kauli inayotumiwa na nchi za Magharibi kwa lengo la kuondoa ushawishi wa China barani Afrika, na inatakiwa kupingwa kithabiti.

Bw. Zindoga ameeleza kuwa, propaganda hizo zimeonesha kuwa nchi za Magharibi hazipendi kuona China inachukua nafasi zao na hivyo kujaribu kuchochea mzozo kati ya China na nchi na watu wa Afrika. Amesema kutokana na nadharia mpya ya maendeleo ya China, China inachukua nafasi za Uingereza na nchi nyingine za Magharibi katika ushirikiano wa kiuchumi na kisiasa, ambapo nchi za Magharibi hazina la kufanya, na propaganda ni moja kati ya chombo chao, vingine ni pamoja na kuiwekea vikwazo nchi huru ikiwemo Zimbabwe, na kuunga mkono mapinduzi ya serikali zinazoshirikiana na China.

Bw. Zindoga amesema kuwa, kuikashifu China kuwa “Mkoloni Mamboleo” kumeonesha pia ubaguzi wa rangi wa nchi za Magharibi, kwani huwa wanaichukua Afrika kuwa ni bara lisilokuwa na maendeleo ya kiakili, lakini nchi za Afrika, iwe ni sehemu ya Umoja wa Afrika au nchi kamili, zinaichukulia China kama ni mshirika kwa sababu zina uwezo wa kutoa sauti zao zenyewe.