Kupambana na ukatili wa watoto na wanawake mtandaoni
2024-01-12 08:10:16| CRI

Matumizi mabaya ya mtandao na mitazamo mingine hasi huathiri ufikiaji na utumiaji wa teknolojia kwa watoto na wasichana na huathiri hali ya kujiamini kwao. Mifumo dume au wakibaguzi wa kijinsia iliyokita mizizi, upendeleo na mitazamo fulani inaathiri uwezo wa wasichana na wanawake vijana kutumia mitandao, kuathiri shughuli zao za mtandaoni na kuathiri ufikiaji wao wa habari na kazi.

Hii inasababisha wasichana kuweka kinga zaidi na kuwa na tabia ya kihafidhina wanapoungana na wengine na kupeana habari za kibinafsi mtandaoni. Mitazamo kama hii haiathiri tu upatikanaji na matumizi ya mitandao kwa wasichana, bali pia inaathiri kujiamini kwao na kuunda mitazamo yao wenyewe ya uwezo wao wa kutumia zana hizi kutekeleza masilahi yao ya kijamii, kielimu na kiakili. Hivyo leo katika kipindi cha ukumbi wa wanawake tutawaelezea mapambano yanayoendelea ya kupinga na ukatili wa watoto na wanawake mtandaoni.