Tunisia kutoa stempu ya kuadhimisha miaka 60 ya uhusiano na China
2024-01-10 08:25:43| CRI

Shirika la Habari la Tunisia TAP limeripoti kuwa nchi hiyo itatoa stempu leo Jumatano kuadhimisha miaka 60 tangu Tunisia na China zianzishe uhusiano wa kibalozi.

Stempu hiyo itapatikana katika ofisi zote za posta kote nchini Tunisia na vilevile kwenye tovuti rasmi ya kutoa stempu hiyo ya maadhimisho.

Tangu China na Tunisia zilipoanzisha uhusiano wa kibalozi Januari mwaka 1964, ushirikiano kati ya nchi hizo mbili umeendelea kukua na kustawi kwenye sekta mbalimbali, ikiwemo afya, michezo, vijana, teknolojia na uvumbuzi.