Marais wa China na Tunisia wabadilishana salamu za pongeza katika kuadhimisha miaka 60 ya uhusiano wa kidiplomasia
2024-01-10 16:03:05| cri

Rais wa China Xi Jinping amemtumia salamu za pongeza rais wa Tunisia, Kais Saied, katika maadhimisho ya miaka 60 tangu kuanzishwa kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo.

Katika ujumbe wake, rais Xi amesema China na Tunisia, zenye urafiki wa jadi, zimeshuhudia ukuaji wa utulivu na imara wa uhusiano wa pande mbili tangu zilipoanzisha uhusiano wa kidiplomasia miaka 60 iliyopita, bila ya kujali mazingira ya kimataifa.

Amesema anatilia maanani sana maendeleo ya uhusiano kati ya China na Tunisia, na yuko tayari kufanya kazi na mwenzake wa Tunisia kuendeleza zaidi uhusiano wa ushirikiano kati ya nchi hizo mbili rafiki.