UM wafuatilia watu laki 5 waliokimbilia Sudan Kusini kutoka Sudan
2024-01-10 09:07:35| CRI

Shirika la kibinadamu la Umoja wa Mataifa limesema wana wasiwasi kuhusu makumi ya maelfu ya wakimbizi na wanaorejea kutokana na mgogoro wa Sudan na kuingia Sudan Kusini.

Ofisi ya Uratibu wa masuala ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa (OCHA) imesema zaidi ya watu 50,000 wamevuka mpaka kutoka Sudan katika wiki tatu zilizopita, na wengine maelfu wanasubiri mpakani kuingia Sudan Kusini.

Ofisi hiyo imesema tangu vita vya Sudan vilipoanza mwezi Aprili mwaka jana karibu watu 500,000 wamekimbilia Sudan Kusini. OCHA inahitaji haraka ufadhili wa ziada ili kukidhi mahitaji makubwa ya kibinadamu katika maeneo ya usafiri na kupanga usafiri kwa wanaowasili ili kupunguza msongamano katika vituo vya usafiri.