Mahakama ya Kikatiba ya DRC yathibitisha ushindi wa Rais Tshisekedi katika uchaguzi mkuu
2024-01-10 08:54:07| CRI

Mahakama ya Kikatiba ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) imethibitisha rasmi ushindi wa Rais Tshisekedi katika uchaguzi mkuu wa nchi hiyo Jumanne wiki hii kufuatia matokeo ya upigaji kura wa tarehe 20 Desemba mwaka jana.

Kwa mujibu wa matokeo ya kura yaliyotangazwa na mahakama hiyo, Bw. Tshisekedi amepata asilimia 73.47 ya kura, akifuatwa na mpinzani wake mkuu Moise Katumbi ambaye amepata asilimia 18.08 za kura.

Habari zinasema rais huyu mteule ataapishwa tarehe 20 Januari baada ya mahakama hiyo kuidhinisha matokeo hayo.