Mvuvi apoteza maisha akidaiwa kuliwa na mamba Mtera
2024-01-10 14:13:26| cri

Mkazi wa Kijiji Cha Mtera, Kata ya Migoli, Mkoani Iringa, Hilary Ngatunga amefariki dunia baada ya kuvamiwa na mamba wakati akivua samaki katika Bwawa la Mtera.

Hili ni tukio la pili kutokea katika kipindi kisichozidi mwezi mmoja ambapo, Disemba mwaka Jana, Mwenyekiti wa Kitongoji cha Chapuya, Kata ya Migoli alipoteza maisha baada ya kuliwa na mamba wakati akivua samaki kwenye bwawa hilo. Diwani wa Kata ya Migoli, Benitho Kayugwa amesema ndani ya mwezi mmoja zaidi ya wavuvi wanne wanadaiwa kuuawa na mamba kwenye bwawa hilo.

Mhifadhi Mwandamizi wa Mamlaka ya Usimamizi wa Wanyamapori (TAWA), Asubuhi Kasuga amesema tayari wameomba kufanyika kwa utafiti kujua idadi ya wanyama waliopo ndani ya bwawa la Mtera ili wavunwe.