Benki ya Dunia: Uchumi wa Afrika kusini mwa Sahara wakua kwa asilimia 2.9 mwaka 2023
2024-01-10 08:48:09| CRI

Benki ya Dunia imetoa ripoti ikisema mwaka jana uchumi wa Afrika kusini mwa Sahara ulikua kwa asilimia 2.9 ikilinganishwa na asilimia 3.7 ya mwaka 2022.

Kwa mujibu wa ripoti ya “Mustakabali wa Uchumi wa Dunia” iliyotolewa na benki hiyo, uchumi wa nchi tatu zinazoongoza kiuchumi katika kanda hiyo - Nigeria, Afrika Kusini na Angola umepungua kwa wastani wa kiwango cha asilimia 1.8 mwaka jana, na kurudisha nyuma ukuaji wa jumla wa kanda hiyo.

Ripoti hiyo pia imesema, ufufukaji wa uchumi baada ya janga la Corona umedhoofishwa kutokana na kupungua kwa mahitaji ya nje na kuimarishwa kwa sera za ndani za kukabiliana na mfumko sugu wa bei.