Rais wa China asema mafanikio ya uhusiano wa China na Marekani yanatokana na juhudi za pamoja za watu wa nchi hizo
2024-01-10 16:03:35| cri

Rais wa China Xi Jinping amesema, mafanikio ya uhusiano kati ya China na Marekani yanatokana na juhudi za pamoja za watu wa nchi hizo mbili.

Rais Xi amesema hayo alipojibu barua ya rafiki yake anayeitwa Sarah Lande anayeishi huko Iowa nchini Marekani.

Amesema hatma ya sayari hii inahitaji utulivu na maboresho ya uhusiano kati ya China na Marekani, kwani China ni nchi kubwa zaidi inayoendelea na Marekani ni nchi kubwa zaidi iliyoendelea duniani.

Pia rais Xi amesema, China iko tayari kufanya kazi na Marekani ili kuendeleza maendeleo endelevu ya uhusiano wa pande mbili.