Wataalamu wa Zambia wapongeza kuanzishwa kwa mfumo wa ufuatiliaji wa taratibu za mauzo ya nje
2024-01-10 08:37:33| CRI

Wataalamu nchini Zambia wamekaribisha uamuzi wa serikali wa kuanzisha mfumo unaolenga kuvutia mapato ya mauzo ya nje ya nchi, hasa katika sekta ya madini.

Benki Kuu ya Zambia, ilitoa mwongozo kuanzia Januari 1, kutekeleza mfumo wa kielektroniki wa ufuatiliaji wa taratibu za mauzo ya nje, unaowataka wauzaji bidhaa nje kufungua na kudumisha akaunti katika benki za ndani.

Mfumo huo unawaamuru wauzaji bidhaa nje wote wapate nambari ya utambulisho wa kodi kutoka kwa Mamlaka ya Mapato ya Zambia, ambayo itaunganishwa na benki kuu.

Wataalamu wa uchumi wa Zambia wanaona kuwa mfumo huo utaleta mabadiliko makubwa kwa mauzo ya nje ya nchi, na kuwa na matokeo chanya kwenye mahitaji ya dola ya kimarekani.