Baraza la Usalama la UM lapitisha azimio la kulaani mashambulizi ya Houthi katika Bahari ya Shamu
2024-01-11 13:52:43| cri

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa Jumatano lilipitisha azimio la kulaani wanamgambo wa kundi la Houthi kwa kufanya mashambulizi dhidi ya wafanyabiashara na meli za biashara katika Bahari ya Shamu.

Azimio hilo namba 2722 linalaani vikali mashambulizi ya Houthi dhidi ya meli zinazopita Bahari ya Shamu tangu tarehe 19 Novemba 2023, ambapo walishambulia na kukamata meli ya Galaxy Leader na wafanyakazi melini.

Azimio hilo linawataka wanamgambo wa kundi la Houthi wasimamishe mashambulizi yote kama hayo, kitendo ambacho kinazuia biashara ya dunia, kuharibu haki na uhuru wa kusafiri baharini na amani na usalama wa kikanda, pia linawataka kuiachia huru meli ya Galaxy Leader na wafanyakazi wake mara moja.