Rais wa Ecuador asema nchi yake iko katika “hali ya vita” na haitajisalimisha kwa magaidi
2024-01-11 13:54:35| cri

Rais Daniel Noboa wa Ecuador Jumatano alisema Ecuador iko katika “hali ya vita” dhidi ya makundi ya uhalifu ya kigaidi yanayohusiana na usafirishaji wa dawa za kulevya, pia aliapa kuwa Ecuador haitaridhia matakwa yao.

Noboa alipohojiwa na “Radio Canela” huko Quito alisema, Ecuador iko katika mapambano ya silaha yasiyo ya kimataifa. Wanapigania amani ya nchi, pia wanapambana na makundi ya ugaidi yenye watu zaidi ya elfu 20 kwa sasa.

Serikali ya Ecuador Jumanne ilitoa agizo ikiwatambua wanachama wa makundi 22 ya uhalifu kuwa ni “magaidi”, na kutangaza kuwa nchi hiyo inaingia katika hali ya mapambano ya silaha ya wenyewe kwa wenyewe, na kuruhusu vikosi vya silaha kupambana na makundi hayo.