Waziri wa Mambo ya Nje wa China kufanya ziara Misri, Tunisia, Togo, Cote d’Ivoire, Brazil na Jamaika
2024-01-11 16:02:09| cri

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya China, Mao Ning amesema, Waziri wa Mambo ya Nje ya China Wang Yi atafanya ziara katika nchi za Misri, Tunisia, Togo, na Cote d’Ivoire kuanzia tarehe 13 hadi 18 mwezi huu.

Bi. Mao Ning amesema, huu ni mwaka wa 34 ambapo Afrika imekuwa kituo cha kwanza cha ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China nje ya nchi kila mwaka.

Ameongeza kuwa, baada ya ziara hiyo barani Afrika, Wang Yi atafanya ziara katika nchi za Brazil na Jamaica kuanzia tarehe 18 hadi 22 mwezi huu.