Waziri wa mambo ya nje wa China atoa wito kuimarisha uratibu wa kimkakati kati ya China na Russia
2024-01-11 08:36:35| CRI

Waziri wa Mambo ya Nje wa China Bw. Wang Yi amesema, China na Russia zikiwa ni nchi kubwa zinazowajibika, zinapaswa kuimarisha mawasiliano ya kimkakati, kupanua zaidi makubaliano ya kimkakati na kuendeleza zaidi ushirikiano wa kimkakati kuhusu mustakbali wa binadamu na dunia.

Bw. Wang Yi ametoa kauli hiyo alipozungumza kwa njia ya simu na mwenzake wa Russia Bw. Sergei Lavrov. Bw. Wang amesema huu ni mwaka wa maadhimisho ya miaka 75 ya uhusiano wa kibalozi kati ya China na Russia, na pia ni mwanzo wa Miaka ya Utamaduni kati ya China na Russia. Amesema pande hizo mbili zinapaswa kufuata makubaliano yaliyofikiwa na wakuu wa nchi mbili, kuandaa shughuli za sherehe, kuongeza mawasiliano ya ngazi ya juu, kuhimiza maendeleo ya kina ya ushirikiano wa kiutendaji, kuendeleza mawasiliano kati ya watu kwenye nyanja mbalimbali, na kuimarisha zaidi uungaji mkono wa umma na msingi wa kijamii kwa uhusiano wa nchi hizo mbili.