Mwakilishi mpya wa UNDP aahidi kuunga mkono maendeleo endelevu ya Ethiopia
2024-01-11 09:58:29| CRI

Mwakilishi mpya wa shirika la mpango wa maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP) nchini Ethiopia Bw. Samuel Gbaydee Doe ameahidi kuunga mkono juhudi za Ethiopia kutimiza lengo la maendeleo endelevu.

Bw. Doe amesema anaona heshima kubwa kuiongoza UNDP Ethiopia katika wakati huu muhimu kwenye historia ya nchi na safari ya maendeleo endelevu.

Ameongeza kuwa shirika hilo litafanya juhudi kujijenga kwenye msingi wa ushirikiano thabiti na wa kudumu kati ya UNDP na serikali na watu wa Ethiopia, ili kuharakisha utimizaji wa matarajio ya maendeleo endelevu kama ilivyoainishwa katika Mpango wa Maendeleo wa Miaka Kumi wa Ethiopia (2021-2030) na mpango wa mageuzi ya kiuchumi.