Watu zaidi ya laki moja nchini Tanzania wagundulika na VVU 2023
2024-01-11 11:07:31| cri

Waziri wa Afya wa Tanzania Ummy Mwalimu amesema watu 163, 131 wamegundulika kuwa na maambukizi mapya ya virusi vya ukimwi (VVU) nchini humo kwa mwaka 2023.

Ummy ameyasema hayo Januari 10, 2023 jijini Dar es Salaam akitoa taarifa ya hali ya utoaji huduma za afya nchini humo kwa mwaka 2023. Amesema, jumla ya watu 8,145,576 walipima Virusi vya UKIMWI (VVU) na Watu 163,131 kati yao walingundulika kuwa na maambukizi ya virusi hivyo.

Aidha, amesema waliokuwa wanatumia dawa za kufubaza virusi vya VVU walikuwa 1,663,651 kulinganisha na watu 1,612,512, huku vifo vitokanavyo na UKIMWI kwa mwaka 2023 vilikuwa 22,000 kulinganisha na vifo 29,000 mwaka 2022. Waziri Ummy amesema kwa ujumla serikali imeendelea kudhibiti maambukizi ya ugonjwa huo.