China na Sierra Leone zaahidi ushirikiano dhidi ya magonjwa ya kuambukiza
2024-01-11 08:51:53| CRI

China na Sierra Leone zimesema zitaendelea kuimarisha ushirikiano katika kuzuia na kudhibiti magonjwa ya kuambukiza ili kuboresha maslahi ya raia wa Sierra Leone.

Semina kuhusu magonjwa ya kuambukiza iliyoandaliwa na Kituo cha China cha Kudhibiti na Kuzuia Maradhi cha China (CDC ya China) na Wizara ya Afya na Usafi wa Mazingira ya Sierra Leone, ilifanyika mjini Freetown ikihusisha kundi la wataalam wa afya, watafiti na watunga sera katika uwanja huo.

Mwanaakademia wa Akademia ya Uhandisi ya China anayefanya kazi katika CDC ya China Bw. Xu Jianquo amesema magonjwa ya kuambukiza yanayoibuka yanaleta changamoto kubwa kwa usalama wa afya na maendeleo ya kijamii na kiuchumi nchini Sierra Leone. Hali hii inahitaji utafiti wa kina na uratibu wa uchunguzi, utambuaji wa magonjwa, matibabu na kinga.