Shule iliyojengwa kwa msaada wa China nchini Botswana yafaulu katika mtihani wa kitaifa
2024-01-11 08:51:09| CRI

Shule ya Msingi ya Mmopane iliyojengwa kwa msaada wa China nchini Botswana imeadhimisha Mtihani wa Kumaliza Elimu ya Msingi (PSLE) kwa mara ya kwanza, na kuwa ya kwanza katika wilaya ya Kweneng kusini kwa kufaulisha asilimia 98.3 ya wanafunzi.

Mwaka 2023, wanafunzi 118 walifanya mitihani shuleni hapo, na 116 walifaulu mitihani, huku 46 wakipata daraja A, 30 daraja B na 40 daraja D.

Ili kusherehekea ufaulu wao pamoja na jamii na viongozi wake, walimu na wafanyakazi wa shule hiyo walizunguka wakiwa kwenye msafara wa magari wilayani Mmopane huku wakiwa wamevalia sare. Mwalimu mkuu wa Shule hiyo Bibi Gagoitsiwe Marata, ameushukuru ubalozi wa China nchini Botswana kwa tuzo unazotoa kwa walimu na wanafunzi, ambazo zimewatia moyo wanafunzi kufanya bidii.