China yachangia mahema kwa wakimbizi waliorejea na wahanga wa mafuriko nchini Sudan Kusini
2024-01-11 09:06:13| CRI

China imechangia mahema 8,808 kwa serikali ya Sudan Kusini kwa ajili ya wakimbizi waliorejea kutoka Sudan ambako wamekimbia mgogoro.

Waziri wa mambo ya kibinadamu na usimamizi wa maafa ya Sudan Kusini Bw. Albino Akol Atak amesema asilimia 60 ya mahema hayo yatasambazwa kwa wahanga katika majimbo kumi na maeneo matatu ya utawala na mengine asilimia 40 ni kwa ajili ya wahanga walioko mjini Juba.

Waziri huyu pia amesema msaada huo wa China wa mahema pamoja na msaada wa chakula, ulitolewa mwezi Mei mwaka jana na umeleta faraja na manufaa kwa wakimbizi hao wanaorejea.