Timu za matibabu za China zapongezwa kwa kuendeleza huduma za afya Tanzania
2024-01-11 08:37:46| CRI

Serikali ya Tanzania Jumanne ilitoa shukrani kwa Serikali ya China kwa kutuma timu za matibabu nchini humo kusaidia kuboresha huduma za afya kwa watu wa nchi hiyo.

Mkurugenzi wa Huduma za Matibabu katika Wizara ya Afya ya Tanzania, Paschal Ruggajo amesema, katika miongo sita iliyopita, zaidi ya madaktari 1,500 wa timu za matibabu za China wametumwa nchini Tanzania, wameokoa maisha ya zaidi ya watu milioni 20 wa Tanzania waliopatwa na magonjwa mbalimbali, na pia wamesaidia kuziba mapengo mbalimbali ya kiteknolojia kwenye hospitali za nchini.

Bw. Ruggajo alisema hayo mjini Dar es Salaam alipohutubia hafla ya kuaga timu ya 26 ya madaktari wa China na kukaribisha timu ya 27 kutoka China.