Kituo cha makontena kilichojengwa na China chaanza kufanya kazi katika mji wa Alexandria nchini Misri
2024-01-11 11:05:09| cri

Kituo cha Makontena cha Bandari iliyopo kwenye Bahari ya Abu Qir kilichojengwa na China katika mji wa pwani wa Alexandria, nchini Misri kimeanza kufanya kazi.

Meli ya mizigo ya China "Zhong Gu Ji Lin" ikipakia makontena 2,000 ya kawaida imetia nanga kwenye sehemu iliyokamilika ya kituo hicho Jumanne asubuhi, na kuashiria kufunguliwa rasmi.

Ujenzi wa kituo hicho umefanywa na Kampuni ya Uhandisi ya Bandari ya China (CHEC) kuanzia mwezi Machi mwaka 2021. Mkuu wa CHEC Misri Duan Kun amesema kuwa awamu yake ya kwanza ilitolewa mwezi Oktoba mwaka 2023, akiongeza kuwa ujenzi huo sasa uko katika awamu ya pili. Ujenzi wa jumla ni pamoja na bandari, uchimbaji, ukarabati, uboreshaji wa njia, kuimarisha ukingo na ujenzi wa vifaa vya kusaidia.

Mradi huo hadi sasa umetoa nafasi za ajira zaidi ya elfu 2 kwa soko la ndani la ajira. Baada ya kujengwa kikamilifu, kituo hicho kitaweza kushughulikia makontena milioni 2 ya kawaida kwa mwaka.