Thamani ya Shilingi ya Kenya dhidi ya Dola ya Marekani yaendelea kushuka
2024-01-12 08:36:37| CRI

Thamani ya Shilingi ya Kenya imeendelea kupungua na kufikia shilingi 160 dhidi ya Dola ya Marekani, na hivyo kutoa shinikizo kwa akiba ya fedha za kigeni ya Kenya na kuongeza gharama ya uagizaji bidhaa kutoka nje.

Benki Kuu ya Kenya (CBK) imesema kwenye biashara ya siku ya Alhamisi, thamani ya sarafu ya nchi hiyo dhidi ya dola ikibadilishwa kwa shilingi 159.8 ikiwa imeshuka kwa takriban asilimia 27 kwa mwaka hadi sasa.

Hadi kufikia Januari 5, akiba ya fedha za kigeni ya Kenya ilikuwa chini ya dola bilioni 6.78, sawa na akiba ya miezi 3.62 tu ya malipo ya uagizaji, ikiwa imepungua kwa takriban dola bilioni 1 kwa mwaka.

Kuporomoka kwa thamani ya shilingi kumetajwa kuwa ni kutokana na kasi ya kubana sera ya fedha kwenye nchi zilizoendelea, ambako kumesababisha kupungua kwa mapato.