Daraja lililojengwa na kampuni ya China mjini Abidjan, Cote d'lvoire lafunguliwa rasmi
2024-01-12 10:16:18| CRI

Daraja moja lililojengwa na Shirika la Uhandisi la Ujenzi la serikali ya China (CSCEC) mjini Abidjan nchini Cote d’lvoire limefunguliwa rasmi Alhamisi wiki hii na linatarajiwa kupunguza msongamano wa magari katika mji huo wakati maelfu ya mashabiki wa mpira wa miguu kutoka sehemu mbalimbali duniani wanapokwenda nchini humo kwa ajili ya Mashindano ya 34 ya Kombe la Mataifa ya Afrika.

Waziri mkuu wa Cote d’lvoire Robert Beugre Mambe alipofanya ukaguzi wa daraja hilo Jumatano wiki hii, alitaja ujenzi wa daraja hilo kuwa mpango muhimu wa miundombinu na lina maana kubwa katika kuboresha hali ya usafiri mjini Abidjan na kuhimiza maendeleo ya uchumi wa mji huo na hata nchi nzima.