Mauzo ya magari ya China katika nchi za nje yaweka rekodi ya juu mwaka 2023
2024-01-12 10:49:37| CRI

Takwimu zilizotolewa jana na Shirikisho la Utengenezaji wa Magari la China (CAAM) zimeonesha kuwa, kutokana na kampuni za magari nchini China kuongeza biashara nje ya nchi, mauzo ya magari ya China katika nchi za nje mwaka 2023 yaliongezeka kwa asilimia 57.9 kuliko mwaka 2022, na kuweka rekodi ya juu ya magari milioni 4.91.