WHO yaonya kuongezeka sana kwa kina cha maji kwenye Mto Congo hadi kwenye kingo
2024-01-12 10:48:14| CRI

Shirika la Afya Duniani (WHO) Alhamisi lilisema kutokana na kuongezeka sana kwa kina cha maji kwenye Mto Congo hadi kukaribia kuvuka kingo, majimbo 9 kati ya 12 za Jamhuri ya Congo zinakabiliana na mafuriko. Pia limetoa tahadhari kuwa watu zaidi ya laki 3.36 wa nchi hiyo wameathiriwa na mvua kubwa.

Ofisi ya WHO inayoshughulikia mambo ya Afrika iliyoko Brazzaville, mji mkuu wa Jamhuri ya Congo ilisema, maeneo 34 na mashamba hekta zaidi ya 2,200 yameathiriwa na mafuriko, na kutenga dola laki moja za kimarekani kwa ajili ya usambazaji wa watu wa huduma ya kwanza.