Kenya yawatafuta wawekezaji wa China kwa ajili ya kuinua nguvu ya ushindani katika sekta ya viwanda
2024-01-12 10:46:49| CRI

Katibu mkuu wa Wizara ya Kuhimiza Uwekezaji ya Kenya Bw. Abubakar Hassan Abubakar Alhamisi alisema, Kenya inafurahia kuwavutia wawekezaji wa China ili kuinua nguvu yake ya ushindani katika sekta ya viwanda.

Abubakar alisema wawekezaji wa China wanatarajiwa kuleta teknolojia ya kisasa, ambayo itaifanya Kenya iweze kutengeneza bidhaa zenye nguvu ya ushindani kwenye soko la dunia. Kenya inataka kutumia utaalamu wa China ili kuufanya msingi wake wa sekta ya viwanda uwe na aina tofauti, ikiwa ni pamoja na bidhaa zenye mahitaji makubwa.

Ameongeza kuwa China imetengeneza teknolojia zao wenyewe, ambazo zinaweza kutumiwa na viwanda vya Kenya kutengeneza bidhaa zinazoweza kukidhi mahitaji ya huko.