Marekani yafanya shambulio dhidi ya maeneo ya kundi la Houthi nchini Yemen
2024-01-12 10:50:50| CRI

Rais wa Marekani Joe Biden amethibitisha kuwa nchi hiyo na wenza wake wamefanya mashambulio katika maeneo yaliyolengwa yanayotumiwa na kundi la Houthi nchini Yemen.

Katika taarifa yake iliyotolewa jana Alhamis, rais Biden amesema mashambulio hayo yalifanywa kwa pamoja na Uingereza na kuungwa mkono na Australia, Bahrain, Canada na Uholanzi, na kuongeza kuwa, mashambulio hayo yalikuwa ni majibu ya mashambulio yaliyofanywa na kundi la Houthi dhidi ya meli za kimataifa zinazosafiri kwenye Bahari ya Shamu.

Marekani imekuwa ikiwaonya wapiganaji wa kundi la Houthi dhidi ya mashambulizi yanayoendelea ya kundi hilo katika meli za kibiashara zinazotumia Bahari ya Shamu.