Benki ya Namibia yajiunga na vuguvugu la kimataifa la ufadhili wa kijani kwa ukuaji endelevu
2024-01-12 08:37:40| CRI

Benki Kuu ya Namibia (BoN) imejiunga na Mtandao wa Kuweka Mfumo wa Kifedha wa Kijani (NGFS), hatua inayolenga kuimarisha usimamizi wake wa hatari za mazingira na hali ya hewa katika sekta ya fedha.

Mtandao huo, kundi la benki kuu na mamlaka za usimamizi zilizojitolea kuhimiza mienendo ya ukuaji endelevu, hivi karibuni waliochagua Benki ya Namibia kuwa mwanachama wake. Hadi kufikia Desemba 27, mwaka jana mtandao huo ulikuwa na jumla ya wanachama na waangalizi 134 na 21 mtawalia.

Gavana wa Benki Kuu ya Namibia Bw. Johannes Gawaxab amesema benki yake kujiunga na mtandao wa NGFS ni hatua muhimu katika kujitolea kwa Namibia katika kuhimiza ukuaji endelevu wa uchumi unaojumuisha juhudi za taifa ambazo zinaipa Namibia nafasi ya kutoa mchango katika jitihada za kimataifa za uondoaji kaboni.