Marekani na Uingereza zafanya mashambulizi mapya dhidi ya Hodeidah nchini Yemen
2024-01-15 09:50:59| CRI

Marekani na Uingereza zimefanya mashambulizi mapya dhidi ya mji wa bandari ya Hodeidah katika Bahari Nyekundu nchini Yemen, wakati ndege za nchi hizo zikiendelea na mashambulizi katika mlima wa Jad'a, wilaya ya Alluheyah kaskazini mwa mji huo.

Mashambulizi hayo ni sehemu ya mfululizo wa mashambulizi yaliyofanywa na ndege za kivita za Marekani na Uingereza katika siku tatu zilizopita.

Marekani na Uingereza zimeeleza kuwa mashambulizi hayo ni hatua za kulizuia kundi la Houthi la Yemen kufanya mashambulizi zaidi dhidi ya meli za kimataifa katika Bahari Nyekundu, ambayo ni njia muhimu ya biashara ya kimataifa.