Waziri Mkuu wa Israel aapa kuendelea na mapambano dhidi ya Hamas wakati mgogoro wa Gaza ukifikia siku 100
2024-01-15 09:57:02| CRI

Wakati mgogoro wa umwagaji damu kati ya Israel na Hamas ukiingia katika siku ya 100, Waziri Mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu ameahidi kuendeleza kampeni ya kijeshi katika Ukanda wa Gaza hadi "ushindi kamili" upatikane.

Bw. Netanyahu amesema lazima waendelee kupambana, na bado itachukua miezi mingi licha ya kuongezeka kwa wito wa kimataifa wa kusitisha vita kutokana na kuongezeka kwa msukosuko wa kibinadamu huko Gaza.

Wakati wa mkutano wake wa kila wiki wa baraza la mawaziri, Bw. Netanyahu aliwasilisha pendekezo la bajeti ya 2024 kwa serikali yake, akitaka kuidhinishwa kwa mpango unaohusisha ongezeko la kodi na utekelezaji wa punguzo la asilimia 3 la bajeti za wizara zote  ili kupata fedha kwa ajili ya operesheni dhidi ya kundi la Hamas.