China yatoa wito wa kuitisha mkutano wa amani wa kimataifa ili kutatua suala la Palestina
2024-01-15 09:52:43| CRI

Waziri wa mambo ya nje wa China Bw. Wang Yi Jumapili ametoa wito wa kuitisha mkutano wa amani wa kimataifa wa pande zote, wenye mamlaka na ufanisi zaidi, ili kuweka mpango wa kutatua mgogoro kati ya Israel na Palestina.

Bwana Wang amesema hayo mjini Cairo kwenye mkutano wa pamoja na wanahabari uliofanyika na waziri wa mambo ya nje wa Misri Sameh Shoukry. Bw. Wang amesema China inaunga mkono katika kurejesha mazungumzo ya amani kati ya Israel na Palestina haraka iwezekanavyo, ili kutimiza kuishi kwa amani kwa pande mbili.

Pia ametoa mapendekezo manne kuhusu kutatua mgogoro huo, ikiwa ni pamoja na kusitisha mapambano huko Gaza haraka iwezekanavyo, na kuheshimu vya kutosha dhamira ya watu wa Palestina kuhusu hatma ya Gaza.