Walinda amani wa UN kuondoka nchini DRC Desemba mwaka huu
2024-01-15 10:43:27| cri

Umoja wa Mataifa umesema, askari wa kikosi cha kulinda amani cha Umoja huo nchini Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) wataondolewa wote kufikia Desemba 2024.

Kiongozi wa Kikosi hicho nchini DRC Bintou Keita amesema, baada ya kikosi hicho kuwepo nchini DRC kwa miaka 25, askari hao watakuwa wameondoka wote itakapofika mwisho wa 2024.

Amesema askari hao wataondoka kwa awamu tatu, na kuongeza kuwa, baadhi ya askari walianza kuondoka nchini DRC mwishoni mwa mwaka jana.