Chama tawala cha Tanzania chateua katibu mkuu mpya
2024-01-16 09:27:31| CRI

Chama tawala cha Tanzania (CCM), kimemteua mwanadiplomasia Dk. Emmanuel Nchimbi kuwa katibu mkuu mpya wa chama hicho kufuatia kujiuzulu kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama hicho Bw. Daniel Chongolo Novemba 2023.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM Bw. Paul Makonda alimtangaza Bwana Nchimbi ambaye ni mwanadiplomasia na aliwahi kuwa waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kuwa katibu mkuu mpya. Bw. Makonda pia aliuambia mkutano na waandishi wa habari mwishoni mwa mkutano wa siku moja wa CCM uliofanyika Zanzibar kuwa Bw. Nchimbi alipitishwa na wajumbe wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya chama hicho baada ya jina hilo kupendekezwa na Kamati Kuu ya chama hicho.