Maofisa wakuu wa nchi wanachama wa harakati ya nchi zisizofungamana na upande wowote (NAM) wanaendelea na mkutano wa siku mbili ulioanza jumatatu, wakitoa mwito suala la mgogoro wa Palestina na Israel kuwa ajenda muhimu.
Mkutano huo ulifunguliwa na naibu waziri wa Mambo ya Nje wa Azerbaijan na mkuu wa ujumbe wa nchi hiyo kwenye mkutano huo Bw. Yalchin Rafiyev, ambaye alizitaka nchi wanachama kuendelea kuwa na umoja wakati dunia ikiendelea kukumbwa na changamoto zenye utatanishi.
Kwenye mkutano huo Balozi wa Palestina kwenye Umoja wa Mataifa Bw. Riyad Mnasour aliwataka wajumbe wa mkutano huo kujadili mgogoro kati ya Palestina na Israel, na kusema kuwa licha ya kuwa Harakati hiyo inakumbana na changamoto nyingi, mgogoro huo wa mashariki ya kati ni wa haraka zaidi.