Korea Kaskazini yaamua kuvunja mashirika yanayoshughulikia ushirikiano kati yake na Korea Kusini
2024-01-16 09:32:26| CRI

Shirika la habari la Korea Kaskazini (KCNA) limeripoti kuwa Korea Kaskazini imeamua kuvunja mashirika yanayoshughulikia ushirikiano kati yake na Korea Kusini.

Ripoti ya KCNA imesema Mkutano wa Ngazi ya Juu wa Baraza la Umma la Korea Kaskazini umetoa uamuzi wa kuvunja Kamati ya muungano wa amani ya nchi, Idara ya ushirikiano wa kiuchumi ya nchi, na Idara ya utalii wa kimataifa ya Kumgangsan, mashirika ambayo yanalenga kuhimiza mazungumzo, majadiliano na ushirikiano kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini.

Ripoti imesema uamuzi huo unatolewa kutokana na Korea Kusini kupanga muungano wa kuifunika Korea Kaskazini na muungano chini ya demokrasia ya kiliberani kuwa sera yake ya taifa, sera ambayo haitaweza kutimiza muungano kati ya Korea Kaskazini na Korea Kusini.