Kundi la Houthi la Yemen latangaza kuhusika na shambulizi dhidi ya meli ya Marekani
2024-01-16 09:34:23| CRI

Kundi la Houthi la Yemen limesema limeishambulia meli ya Marekani katika Ghuba ya Aden kwa makombora kadhaa.

Msemaji wa jeshi la Houthi Yahya Sarea amesema katika taarifa kwenye televisheni ya al-Masirah inayoendeshwa na kundi hilo, kuwa shambulizi hili lilikuwa "sahihi na la moja kwa moja".

Mapema Jumatatu Kamandi Kuu ya Jeshi la Marekani ilisema meli ya mzigo iliyopeperusha bendera ya Visiwa vya Marshall Gibraltar Eagle, inayomilikiwa na kuendeshwa na kampuni ya usafirishaji ya Marekani ilishambuliwa kwa kombora la Houthi.