Waziri Mkuu wa China asema China itaendelea kushirikiana na Umoja wa Ulaya
2024-01-17 09:57:15| CRI

Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang amesema China iko tayari kushirikiana na Umoja wa Ulaya (EU), na kushughulikia ipasavyo tofauti zilizopo kati ya pande mbili chini ya kanuni ya kuelewana na kuheshimiana.

Bw. Li amesema kwenye dunia ya leo ambayo imejaa mabadiliko na misukosuko, uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya bado upo thabiti katika uhusiano kati ya nchi kubwa, jambo ambalo linatokana na juhudi za pamoja. Bw. Li alisema alipokutana na mwenyekiti wa Kamisheni ya Umoja wa Ulaya Bibi Ursula von der Leyen kando ya Mkutano wa Baraza la Uchumi la Dunia 2024.

Bw. Li amesema Rais wa China Xi Jinping alivyosema, uhusiano kati ya China na Umoja wa Ulaya una umuhimu wa kimkakati na ushawishi wa kimataifa, na kuongeza kuwa kuimarisha uhusiano kati ya China na EU daima ni kipaumbele cha kidiplomasia kwa China.