DRC yaanzisha operesheni za pamoja za kijeshi na ujumbe wa SADC dhidi ya waasi
2024-01-17 09:54:18| CRI

Jeshi la Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) limetangaza mjini Goma, kuanza kwa operesheni za pamoja za kijeshi dhidi ya waasi kwa kushirikiana na vikosi vya Jumuiya ya Maendeleo ya nchi za kusini mwa Afrika (SADC).

Tangazo hilo limetolewa na Luteni Jenerali Fall Sikabwe, mratibu wa operesheni za kijeshi za jeshi la DRC huko Kivu Kaskazini, wakati wa mkutano wa kwanza wa pamoja kati ya jeshi la DRC na SADC. Mamlaka za DRC zimesema jeshi la SADC litafanya operesheni za mashambulizi haswa kulilenga kundi la waasi la M23, ambalo linashikilia maeneo kadhaa katika eneo la Masisi na Rutshuru, katika jimbo la Kivu Kaskazini.

Kikosi cha SADC kinaundwa hasa na wanajeshi kutoka Afrika Kusini Tanzania na Malawi, na kinachukua nafasi ya jeshi la kikanda la Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), ambalo mamlaka za DRC ziliona kuwa halifanyi kazi.