Sudan yasitisha mawasiliano na kundi la upatanishi la IGAD
2024-01-17 23:07:18| cri

Sudan imesitisha mawasiliano na Shirika la Maendeleo la Serikali za Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) ambalo limekuwa likifanya juhudi za upatanishi kati ya jeshi la Sudan na kikosi cha RSF, ambayo yamekuwa katika mapigano makali kwa miezi kadhaa sasa.

Taarifa iliyotolewa na Wizara ya Mambo ya Nje ya Sudan imesema, IGAD ilijitolea kuwa mpatanishi kati ya kiongozi wa Jeshi la Sudan na kiongozi wa kikosi cha RSF, ikiwemo kuwa mwenyeji wa mkutano, ambapo pande zote mbili zilikubali.

Taarifa hiyo imekuja saa 47 kabla ya kuitishwa kwa mkutano maalum uliopangwa kufanyika mjini Entebbe, Uganda, kujadili vita inayoendelea nchini Sudan.

Hata hivyo, Sudan ilisema haitahudhuria mkutano huo kwa kuwa IGAD imemwalika kiongozi wa kikosi cha RSF, Jenerali Mohamed Hamdan Daglo.