Askari wawili wa jeshi la Marekani hawajulikani walipo baada ya operesheni karibu na Somalia
2024-01-17 09:51:18| CRI

Kamandi kuu ya jeshi la Marekani (CENTCOM) imesema askari wawili wa jeshi la baharini la Marekani hawajulikani walipo kwenye operesheni ya hivi karibuni iliyofanywa na jeshi la Marekani karibu na pwani ya Somalia ili kukamata silaha za Iran kwa ajili ya Kundi la Houthi la Yemen.

Taarifa iliyotolewa na kamandi hiyo, imesema askari hao wawili walikuwa wanafanya operesheni ya usiku wa tarehe 11 Januari, operesheni ambayo inalenga kukamata “jahazi linalosafirisha kiharamu vifaa vya msaada vinavyoweza kusababisha vifo kutoka Iran kwenda kwa vikosi vya Houthi nchini Yemen, ambavyo ni sehemu ya kampeni ya mashambulizi ya Houthi dhidi ya meli za biashara za kimataifa”.

Kamanda wa CENTCOM Michael Kurilla amesema kazi ya upekuzi inafanyika ili kuwatafuta askari hao wawili.