Waziri mkuu wa China atuma salamu za pongezi kwa mwenzake wa Ufaransa
2024-01-17 14:00:52| cri

Waziri Mkuu wa China Bw. Li Qiang jana Jumanne ametuma salamu za pongezi kwa Bw. Gabriel Attal kwa kuteuliwa kuwa Waziri Mkuu wa Ufaransa.

Bw. Li Qiang amesema, China na Ufaransa zote ni nchi wajumbe wa kudumu wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na pia ni nchi kubwa zinazojiamulia mambo yake. Amesema katika miaka ya karibuni, chini ya uongozi wa kimkakati wa wakuu wa nchi hizo mbili, uhusiano kati ya China na Ufaransa umeendelea kupiga hatua, hali inayoleta utulivu katika dunia inayoshuhudia sintofahamu na mabadiliko makubwa. Amesema, mwaka huu ni maadhimisho ya miaka 60 tangu China na Ufaransa zianzishe uhusiano wa kibalozi, na anapenda kushirikiana na mwenzake wa Ufaransa katika kutoa msukumo mpya kwenye mawasiliano na ushirikiano wa pande mbili, na kutoa mchango mpya katika kujenga Uhusiano wa Wenzi wa Kimkakati wa Pande Zote ulio tulivu, wenye kunufaishana na kupanua nyanja mpya kati ya nchi hizo mbili.