Wanasayansi wa Kenya wazindua dawa ya kupunguza malaria miongoni mwa wanawake wajawazito walio na VVU
2024-01-17 09:55:28| CRI

Dawa mpya inayotarajiwa kupunguza maambukizi ya malaria miongoni mwa wanawake wajawazito wanaoishi na VVU, ilitolewa Jumanne na wanasayansi wa Kenya na Malawi kufuatia majaribio makini.

Kupitia matokeo ya utafiti yaliyochapishwa katika jarida la linaloheshimiwa la Lancet, wanasayansi wamebainisha kuwa kuongezwa kwa dawa ya kutibu malaria (dihydroartemisinin-piperaquine) kwenye orodha ya dawa nyingine zilizopo, kutapunguza kwa kiasi kikubwa hatari ya kuambukizwa malaria miongoni mwa wanawake wajawazito wanaoishi na VVU.

Kaimu mkurugenzi mkuu wa Taasisi ya Utafiti ya Matibabu ya Kenya (KEMRI), Bw. Elijah Songok amesema hayo ni mafanikio makubwa yanayoongoza dawa dhidi ya ugonjwa unaohatarisha takriban asilimia 70 ya maisha ya wagonjwa.