China na Algeria zaahidi kuendelea kuungana mkono na kushirikiana
2024-01-17 09:49:43| CRI

China na Algeria zimeahidi kuendelea kuungana mkono katika masuala yanayohusiana na maslahi makuu na kuimarisha ushirikiano katika nyanja mbalimbali.

Ahadi hiyo imetolewa wakati wa ziara ya naibu waziri mkuu wa China ambaye pia ni mjumbe wa Ofisi ya Siasa ya Kamati Kuu ya Chama cha Kikomunisti cha China Bw. Liu Guozhong, ambaye Jumanne alikutana na Rais Abdelmadjid Tebboune wa Algeria na Waziri Mkuu Nadir Larbaoui mjini Algiers.

Katika mikutano hiyo Bw. Liu alipongeza maendeleo iliyopata Algeria, akisema China na Algeria ni "marafiki wa dhati na washirika wa asili wa maendeleo ya pamoja na ustawi wa taifa." Amesema huu ni mwaka wa 10 tangu nchi hizo mbili zianzishe ushirikiano wa kina wa kimkakati, na China inapenda kutumia fursa hii kushirikiana na Algeria na kuhimiza ushirikiano chini ya utaratibu wa ujenzi wa pamoja wa hali ya juu wa Ukanda Mmoja, Njia Moja.

Rais Tebboune na waziri mkuu Larbaoui wamesema kuimarisha ushirikiano na China ni chaguo la kimkakati kwa Algeria, wakiahidi kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa pamoja wa BRI, na kuvutia kampuni za China kuwekeza Algeria.