Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa lalaani shambulio baya dhidi ya tume ya Umoja huo nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati
2024-01-18 10:41:58| cri

Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa limelaani vikali shambulio dhidi ya Tume ya Umoja wa Mataifa nchini Jamhuri ya Afrika ya Kati lililotokea jumatatu na kusababisha kifo cha askari mmoja wa kulinda amani kutoka Cameroon na wengine watano kujeruhiwa.

Rais wa Baraza hilo ambaye ni Balozi wa Ufaransa katika Umoja wa Mataifa Nicolas de Riviere ametoa salamu za rambirambi kwa familia ya askari aliyeuawa na kwa taifa la Cameroon.

Nchi wajumbe wa Baraza hilo wameeleza kusikitishwa na shambulio hilo, na kusema mashambulio dhidi ya askari wa kulinda amani ni sawa na uhalifu wa kivita, na kusisitiza pande zote husika kutimiza wajibu wao chini ya sheria ya kimataifa ya kibinadamu.