Umoja wa Afrika watoa wito kwa Ethiopia, Somalia kujizuia na kupunguza mvutano
2024-01-18 10:10:15| CRI

Umoja wa Afrika (AU) umetoa wito kwa Ethiopia na Somalia kujizuia na kuchukua hatua za kupunguza mvutano uliopo na kuzorota kwa uhusiano wa kidiplomasia kati ya nchi hizo mbili.

Wito huo umetolewa na Baraza la Amani na Usalama la Umoja wa Afrika katika taarifa iliyotolewa kufuatia mkutano wake uliofanyika Jumatano, ulioangazia hali ya sasa ya uhusiano kati ya Ethiopia na Somalia, na utatuzi wa amani wa suala hilo kwa moyo wa masuluhisho ya Kiafrika kwa matatizo ya Kiafrika.

Umoja wa Afrika umezihimiza nchi hizo mbili kujiepusha na vitendo zaidi na kauli zinazoweza kuathiri vibaya ukaribu uliopo kati ya nchi hizo mbili.

Baraza hilo pia limeonesha "wasiwasi wake mkubwa" kuhusu mvutano unaoendelea kati ya nchi hizo mbili na athari zinazoweza kutokea kwa amani, usalama na utulivu wa eneo hilo.