Ofisi ya Umoja wa Mataifa Inayoratibu Masuala ya Kibinadamu (OCHA) imeeleza wasiwasi wake mkubwa kuhusu hali inayozidi kuwa mbaya katika maeneo yaliyoathiriwa na ukame kaskazini mwa Ethiopia, ikiwa ni pamoja na mikoa ya Amhara, Oromia, Afar na Tigray.
OCHA imesema, mamilioni ya watu wako hatarini kukabiliwa na mahitaji makubwa ya msaada wa kibinadamu na umasikini, na kwamba wenzi wa kibinadamu wanaungana na serikali ya Ethiopia kuwasaidia watu hao licha ya changamoto za kimazingira, hususan katika maeneo yanayokabiliwa na machafuko katika mikoa ya Amhara na Oromia.
Ofisi hiyo imesema, mashirika ya kibinadamu yamewasaidia watu zaidi ya milioni 12 kati ya mwezi Januari hadi Novemba mwaka jana.