Waziri wa mambo ya nje wa China afanya ziara ya kwanza ya mwaka mpya barani Afrika kwa miaka 34 mfululizo
2024-01-18 11:11:13| CRI

Hujambo msikilizaji na karibu tena kwenye kipindi cha Daraja kinachokujia kila jumapili muda kama huu kupitia CMG Idhaa ya Kiswahili inayokutangazia kutoka hapa Beijing.

Katika ripoti yetu ya leo, tutakufahamisha mambo yaliyojitokeza katika ziara ya Waziri wa Mambo ya Nje wa China barani Afrika, ikiwa ni utamaduni uliodumu kwa miaka 34 sasa. Pia tutakuwa na mahojiano kutoka CMG Idhaa ya Kiswahili Nairobi itakayohusu kuongezeka kwa wanachama wa Kundi la BRICS na kufikia 11.