Mawaziri wa Mambo ya Nje wa Kenya na Tanzania wajadili changamoto ya ustawi wa biashara
2024-01-18 10:42:58| cri

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki wa Tanzania, January Makamba, amekutana na Waziri Mkuu na Waziri wa Mambo ya Nje na Diaspora wa Kenya, Dkt. Musalia Mudavadi jijini Kampala, Uganda.

Mawaziri hao wamekutana nchini Uganda kando ya Mkutano wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa Nchi Zisizofungamana na Upande Wowote (NAM).

Katika mkutano huo, mawaziri hao wamejadili masuala mbalimbali ya kuimarisha ushirikiano kati ya nchi hizo mbili, na kuahidi kuendelea kutumia majukwaa ya kidiplomasia kutatua changamoto mbalimbali, zikiwemo zile zinazokwamisha ustawi mzuri wa biashara, uwekezaji, utalii na uendelezaji wa miundombinu kwa manufaa ya pande zote mbili.